SERIKALI YAENDELEA KUBORESHA UTENDAJI SEKTA YA NISHATI


 Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imeendelea kuhakikisha kila sekta  inakuwa katika ubora unaostahili, na hili limedhihirika katika maeneo mbalimbali ikiwemo sekta ya nishati nchini.

 

Katika kuthibitisha hilo, Januari, 23 jijini Dodoma, Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko amekutana na Waziri wa Maji, Jumaa Aweso, pamoja na wataalam kutoka Wizara ya Nishati na Wizara ya Maji kujadili namna ya kuboresha utendaji na kukabiliana na changamoto zinazozikabili Taasisi zilizopo chini ya Wizara hizo. 

 

Viongozi hao wateule wa Rais Samia wameketi kujadili hayo ikiwa zimebaki siku 4 tu ili kuanza kwa Mkutano wa Nishati wa Wakuu wa Nchi za Afrika, unaotarajiwa kuanza Januari 27, 2025 katika ukumbi wa JNICC jijini Dar es Salaam.

#KhomeinTvUpdates 

 

️ Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv



Post a Comment

0 Comments