WAKULIMA WAPANDA MITI 1,000 KUUNGA MKONO UTUNZAJI WA MAZINGIRA

 

Wakulima  na wananchi wa mtaa Itezi Mlimani Kata ya Nsalaga Jijini Mbeya wameunga mkono jitihada za serikali kwa kupanda miti 1,000 iliyotolewa na Wakala wa Huduma za Misitu (TFS).

 

Wamesema hatua hiyo ya kupanda miti ni kumpongeza Rais Samia Suluhu Hassan katika kusherehea siku yake ya kuzaliwa Januari 27 mwaka huu kwa kufanya vyanzo vya maji kuwa vya kijani

 

Mkulima Sarah Japhet, amesema wana kila sababu ya kushirikiana na serikali  kuhifadhi na kutunza vyanzo vya maji ambavyo vipo ndani ya misitu ya  hifadhi ya TFS.

 

"Awali katika eneo tulilopewa kwa ajili ya kilimo lilikuwa chini na TFS na tulikuwa na mgogoro uliodumu miaka nane lakini tunaishukuru serikali kupitia Mbunge na Spika wa Bunge Dkt,Tulia Ackson kufanya mazungumzo  na hatimaye tumerejeshewa ,"amesema.

 

Mwenyekiti wa Mtaa wa Itezi mlimani ,Tegemeo Moto anaishukuru serikali kupitia Wakala wa Huduma za Misitu ( TFS) kwa kutoa miti kwa ajili ya kupanda kwenye vyanzo vya maji ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.

 

"Tunaona mabadiliko ya tabia nchi yanavyo athiri shughuli za kilimo kufuatia shughuli za kibinadamu na ukataji miti ovyo ,kupitia zoezi hilo la upandaji miti tunakwenda kuwa wasimamizi ili kurejesha mvua na uoto wa asili kwenye vyanzo vya maji,"amesema.

 

Kaimu mtendaji wa mtaa wa Itezi Mlimani Ezra Chaula ,amesema wanaishukuru serikali kwa kuridhia sehemu ya eneo hilo kurejeshwa kwa wananchi kwa ajili ya kilimo na kuwataka kutofanya uharibifu wa kulima ndani ya mita 60 ya vyanzo vya maji.

 

" Tunamshukuru Mbunge wa Mbeya Mjini na Spika wa Bunge kukutana na pande zote mbili hatimaye TFS  kurejesha wananchi sehemu ya eneo  kwa ajili ya kuendeleza kilimo,"amesema.

 

Chaula ameomba TFS kuendelea kutoa miti kwa  wakulima ili kuendeleza kampeni ya upandaji miti kwenye vyanzo vya maji kwa lengo la kutunza mazingira na kudhibiti athari ya  mmonyoko wa udongo.

 

Katibu wa kikundi cha Wakulima hao, Crispin Kandi amesema kitendo cha TFS kuridhia kurejesha eneo la kilimo kwao  wameonyesha uzalendo wa kuwajali wananchi ambao  hutegemea safu ya mlima huo kuzalisha mazao ya kilimo na biashara.

 

Mhifadhi Mkuu wa shamba la miti Kawetire  linalosimamiwa na Wakala wa Huduma za Misitu (TFS) ,  Arnold Shoo amesema katika kuhakikisha wananchi wanatunza mazingira wataendelea kutoa miti ya aina mbalimbali.



 

"Tumetoa miti zaidi ya 1,000 kwa wakulima wa eneo hilo lengo ni kuona wanatunza mazingira katika safu ya Mlima Kawetire  kwa ajili ya kutunza uhifadhi wa miti na  vyanzo vya maji ili  kudhibiti mmonyoko wa udongo unaotokana na shughuli za kilimo "amesema Shoo.

 

Awali , Shoo amesema  anashukuru serikali kupitia uongozi wa juu wa TFS na Spika wa Bunge na Mbunge wa Mbeya Mjini, Dkt. Tulia Ackson kuridhia sehemu ya eneo kurejesha kwa wananchi kwa ajili ya kilimo .

 

Wakati huo huo, Shoo amewataka wananchi wanaolima kwenye  maeneo ya hifadhi za misitu kuacha tabia na uchomaji ovyo moto pindi wanapoandaa mashamba na badala yake watumie askari wa TFS ili kudhibiti majanga ya moto yanayojirudia mara kwa mara na kusababisha hasara.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

️ Mwandishi wetu-Mbeya

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Post a Comment

0 Comments