Shirika la Ndege la Tanzania (ATCL) limerejesha huduma za usafiri wa ndege za shirka hilo mkoani Mtwara, ambapo ndege hizo zitakuwa zikifanya safari za Dar es Salaam-Mtwara mara Tatu kwa wiki.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL) Arif Jihann, akizungumza leo Februari 17, 2025 katika uzinduzi wa safari hizo mkoani Mtwara, amesema Mtwara inanafasi muhimu katika uchumi wa Tanzania kutokana na rasilimali zilizopo.
Jihann amesema kurejeshwa kwa safari za usafiri wa anga kupitia ndege za Air Tanzania, kutachochea ukuaji wa sekta ikiwemo uwepo wa nishati ya gesi, uvuvi, kilimo biashara na utaliii wa fukwe.
Meneja wa Uwanja wa Ndege wa Mtwara Jordan Mchami amesema kutokana na kuwepo kwa gharama ndogo za nauli kwenda na kurudi kutoka Mtwara kwenda Dar es Salaam ambayo ni shilingi 199,000, kutapelekea kuongezeka kwa abiria watakaotumia usafiri huo.
"Hapo awali tulipokuwa na Shirika Moja la Ndege nauli ilikuwa Sh 300,000 mpaka zaidi ya 400,000 maana yake ni hakukuwa na ushindani " amesema Mchami.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mtwara Abdallah Mwaipaya, ambaye ndio amezindua safari hizo katika kiwanja cha ndege cha Mtwara, amesema uamuzi wa kurejeshwa safari hizo sio tu zitafungua milango mipya kwa Mtwara kama kitovu muhimu cha biashara, uwekezaji na utalii lakini zitatatua changamoto kubwa za usafiri wa anga ambazo wakazi wa Mtwara na mikoa jirani wamekuwa wakizikabili kwa muda mrefu.
"Kurejea kwa Air Tanzania hapa Mtwara kumerahisisha urahisi wa safari na mmeweka nauli punguzo maalum la Sh 199,000 kwa safari ya kwenda na kurudi "amesema Mwaipaya.
#KhomeinTvUpdates
✍️Zamzam Jambia-Mtwara
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments