SERIKALI YAKERWA WATOTO KUSOMEA CHINI YA MITI|WAKURUGENZI WAWEKWA KIKAANGONI

 

Serikali ya Rais Samia Suluhu Hassan imeagiza kufanyika kwa  tathmini ili kubaini maeneo ambayo wanafunzi wanalazimika kusoma chini au kukaa chini ya miti, kutokana na uhaba wa vyumba vya madarasa.

 

Agizo hilo limetolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Mohamed Mchengerwa.

 

Mchengerwa pia amewataka wakurugenzi wa halmashauri na wataalamu wao kuandikiwa barua za kujieleza juu ya hali hiyo.

 

Agizo hilo limetolewa hivi karibuni, jijini Dodoma, wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya kukabiliana na msongo wa mawazo kazini kwa watumishi wa TAMISEMI.

 


Mchengerwa amesisitiza kuwa haiwezekani katika karne hii wanafunzi wakakosa madarasa au madawati, ilhali serikali imetumia matrilioni ya shilingi kuboresha sekta ya elimu.

 

"Miaka yote tumekuwa tukipata usumbufu ikifika Desemba na Januari, lazima zitafutwe sh. bilioni 250 au 300 kwa madarasa na madawati. Lakini sasa miaka miwili imepita hatujamuomba Rais fedha za kujenga madarasa au kununua madawati. Msisubiri msukumwe, fanyeni kazi," amesisitiza Mchengerwa.

 

Ameagiza Idara ya Usimamizi wa Elimu ya TAMISEMI kufanya tathmini ya shule zote za msingi na sekondari zilizo chakavu ili kuweka mpango wa ukarabati.

 


Aidha, amewapongeza watumishi wa TAMISEMI kwa kusimamia uchaguzi wa Serikali za Mitaa kwa ufanisi na kuwataka kuendelea kutoa huduma bora zinazokidhi matarajio ya wananchi.

 

Kuhusu sekta ya afya, Mchengerwa ameeleza kuwa juhudi za TAMISEMI zimechangia kupunguza vifo vya mama na mtoto, huku akihimiza ufuatiliaji wa karibu kwa waganga wakuu wa mikoa na wilaya ili kuboresha huduma za afya kwa wananchi.

 

Aidha, amewahimiza watumishi hao kufuatiliwa kwa karibu Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya na kwenye vituo vya afya ili waongeze kasi ya kuwahudumia wananchi kwa weledi.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments