DARASA LINALOTEMBEA KUWANUFAISHA WANAFUNZI MBEYA

 


Zaidi ya watu 20, 000 wakiwemo wanafunzi wa Shule  mbili za Sekondari Jijini Mbeya  watanufaika na programu ya  kidigali kwa wote itakayo tumia nishati ya  umeme wa jua kupitia darasa linalotembea (Digitruck) kwa kushirikiana na Taasisi ya Tulia Trust.

 

Katibu Tawala Wilaya ya Mbeya, Mohammed Fakii amesema leo Jumanne Februari 11,2025 kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Beno Malisa wakati akizindua programu elimu ya kidigitali kupitia darasa linalotembea(Digitruck)  chini ya mpango wa TECH 4 ALL wa Huawei ambao kwa Tanzania umeanza katika Mkoa wa Mbeya.

 


Fakii amesema kuwa ujio wa programu hiyo itawaongezea ujuzi kwa walimu wa masomo ya tehama na vijana  kutafuta fursa mbalimbali za kiuchumi kwa kutumia mifumo ya kiditali.

 

"Kama tulivyo msikia mwakilishi wa Mkurugenzi wa Digitruck kuwa matarajio ni kuwafikia watu 20,000  kutokana na umuhimu wa matumizi ya teknolojia kwa sasa nilitamani  watu 40,000 wafikiwe na programu hiyo,"amesema.

 


Amesema kwa nchi ya Tanzania ilichelewa kuanza  programu na kwamba ni wakati sasa wananchi kuchangamkia fursa hiyo ambayo inakwenda kufungua wigo mpaka wa fursa za kibiashara na kiuchumi .

 

Fakii amesema programu hiyo ni matunda ya Mbunge wa Mbeya mjini, Dkt Tulia Ackson baada ya kufanya ziara nchini China na kutoa ombi lake la kutaka elimu ya Tehama ifike nchini Tanzania hususani kwa Mkoa wa Mbeya.

 

Akizungumza kwa njia ya mtandao  Spika wa Bunge na Mbunge Mbeya mjini, Dkt Tulia Ackson amesema kwa Tanzania hii awamu ya kwanza na kuzinduliwa kwa Mkoa wa Mbeya katika shule ya sekondari Forest.

 


Amewataka wananchi kutumia fursa hiyo  katika shughuli za kiuchumi, ujasiriamali na ujuzi kwa vijana katika matumizi ya mifumo ya tehama.

 

Mwakilishi wa Mkurugenzi wa Programu ya Digitruck,Bruce Zhao amesema lengo ni kuimarisha ujuzi wa kidigitali kwa vijana na wanawake huku akibainisha ni kuonyesha mashirikiano baina yao  na Taasisi ya Tulia Trust ambayo Mkurugenzi wake Spika wa Bunge, Mbunge wa Mbeya mjini Dkt. Tulia Ackson.

 

"Tunatazama ushirikiano zaidi ili kufanikisha kauli mbiu "In Tanzania, For Tanzania" tunaamini kwa kushirikiana tutafanikisha mambo makubwa kwa mustakabali mzuri wa watanzania wote."amesema.

 

Baadhi ya wanafunzi wa shule zitakazo nufaika na programu hiyo  wamemshukuru Mbunge wa Mbeya mjini ,Dkt Tulia Ackson kwa kuleta mfumo wa tehama kupitia darasa linalotembea ambalo litakuwa mwarobaini  kwao  kwenda na teknolojia ya kisasa ya kidigitali.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️Mwandishi wetu-Mbeya

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments