Serikali ya India kupitia Waziri wa Petroli na Gesi Asilia India Hardeep Singh imeipongeza Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kupiga hatua kubwa kwenye usambazaji wa umeme hususan vijijini.
Hayo yamejiri Februari 11, 2025 jijini New Delhi nchini India, katika Maadhimisho ya Tatu ya Wiki ya Nishati nchini humo.
Aidha, Waziri Singh amempongeza pia Dkt. Biteko kwa hekima zake na ukomavu ambao anauonesha pale anapoieleza dunia kuhusu masuala ya uendelezaji wa rasilimali zinazoweza kuzalisha umeme ambazo Bara la Afrika imebarikiwa nazo lakini mpaka sasa hazijaendelezwa ipasavyo kutokana na misimamo ya kidunia ikiwemo, makaa ya mawe ambayo yakiendelezwa yatazidi kutoa uhakika wa uwepo wa nishati ya kutosha.
Sambamba na kuisifia Serikali ya Tanzania kwa jinsi inavyotekeleza mkakati wa nishati safi ya kupikia kwa namna mbalimbali ikiwemo kuweka ruzuku kwenye mitungi ya gesi.
Maadhimisho hayo yamehudhuriwa pia na Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini ambaye anamwakilisha Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Idd Kassim, Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu Mhandisi Innocent Luoga na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), Dkt. James Andilile.
✍️Mwandishi wetu
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments