UMATI WAMLAKI RAIS SAMIA MKOANI SIMIYU

 



Wananchi wa Mkoa wa Simiyu wamempokea kwa shangwe na nderemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, aliyewasili mkoani humo Juni 15, 2025 kwa ziara ya kikazi.

 

Mara baada ya kuwasili, Rais Samia alionekana akiwa mwenye bashasha, akisalimiana na wananchi waliojitokeza kwa wingi pembezoni mwa barabara kumpokea kwa furaha na heshima kubwa.Mapokezi hayo yameambatana na shamrashamra, pamoja na kauli mbalimbali za kumpongeza kwa kazi zinazofanyika chini ya uongozi wake.

 

Katika ziara yake Rais Samia anatarajiwa pia kuzindua daraja la Kigongo - Busisi lililojengwa juu ya Ziwa Victoria mkoani Mwanza. Daraja ambalo ni moja ya mradi mkubwa mkoani humo, utakaosaidia kukuza kiuchumi kwa maendeleo ya nchi na jamii kwa ujumla.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments