JAJI MBAROUK AFUNGUA MAFUNZO KWA WATENDAJI DAFTARI LA WAPIGA KURA

 

Mteule wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Makamu Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Rufaa (Mst) Mbarouk Salim Mbarouk amefungua mafunzo kwa watendaji wa Daftari la kudumu la Wapiga Kura mkoani Tanga, huku akiwaasa kutekeleza majukumu yao kwa umakini katika kila eneo ikiwemo utunzaji wa vifaa vya uandikishaji.

 

“Ni muhimu kutekeleza majukumu yenu kwa umakini katika kila eneo ikiwemo utunzaji wa vifaa vya uandikishaji hasa ikizingatiwa kuwa, vifaa hivi vimenunuliwa kwa gharama kubwa sana na vinatarajiwa kutumika katika maeneo mengine ya uandikishaji nchini,” amesema Jaji Mbarouk.

 

Ameongeza kuwa kutokuwa makini katika utunzaji wa vifaa hivyo kutapelekea athari kubwa katika ukamilishaji wa zoezi hilo muhimu, na kwamba wana wajibu wa kuzingatia maelekezo yote yatakayotolewa na Tume ili waweze kuyafanyia kazi wakati zoezi hilo la uboreshaji wa daftari litakapokuwa limeanza kwenye maeneo yao.

 

Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura utafanyika mkoani Tanga na Pwani kwa siku saba kuanzia tarehe 13 hadi 19 Februari, 2025 ambapo vituo vitakuwa vinafunguliwa saa 02:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni.

 

Zoezi hilo ambalo lilizinduliwa mkoani Kigoma mwezi Julai, 2024 limeshakamilika kwenye mikoa 25 ambayo ni Kigoma, Tabora, Katavi, Geita, Kagera, Mwanza, Shinyanga, Mara, Simiyu, Manyara, Dodoma, Singida, Mjini Magharibi, Kusini Unguja, Kaskazini Unguja, Kusini Pemba, Kaskazini Pemba, Arusha, Kilimanjaro, Mbeya, Iringa, Rukwa, Songwe, Njombe na Ruvuma.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️ Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments