Mwenyekiti wa Tume Huru ya Taifa ya Uchaguzi, Jaji Rufaa Jacobs Mwambegele amewataka Watendaji wa Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura mkoani Tanga na Pwani kufanya kazi kwa weledi, bidii na moyo wa kujituma ili kufanikisha zoezi hilo.
Hayo yamejiri jijini Tanga, Februari 02, 2025 wakati akifungua mafunzo ya watendaji wa uboreshaji wa daftari ngazi ya mkoa, mkoani humo.
“Baadhi yenu mlibahatika kushiriki katika kuratibu na kusimamia utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Tume ikiwemo uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura katika awamu zilizopita. Kwa kutumia uzoefu mlionao na mafunzo mtakayopatiwa, ninaamini mtafanya kazi zenu kwa weledi, bidii na moyo wa kujituma ili kufanikisha zoezi hili,” Jaji Mwambegele amewafunda watendaji hao.
Amewataka kutumia uzoefu walionao kuwasaidia wenzao ambao hawakuwahi kushiriki katika zoezi kama hilo ili waweze kutekeleza majukumu yao kikamilifu.
Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura utafanyika mkoani Tanga na Pwani kwa siku saba kuanzia tarehe 13 hadi 19 Februari, 2025 ambapo vituo vitakuwa vinafunguliwa saa 02:00 asubuhi na kufungwa saa 12:00 jioni.
✍️ Mwandishi wetu
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments