JIJI LA DAR KUJENGWA KISASA ZAIDI


 Mteule wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Mohamed Mchengerwa 

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-TAMISEMI amekutana na wawakilishi wa Kampuni ya Straling Holding ya Abu Dhabi na kujadili namna bora ya ujenzi wa mji mpya wa kisasa katika Jiji la Dar es Salaam.

 


Waziri Mchengerwa amekutana na Kampuni  hiyo Februari 14, 2025 katika ukumbi wa TAMISEMI jijini Dodoma, ambao wameonesha nia ya kuwekeza kwenye ujenzi wa miundombinu ya barabara, madaraja, elimu, afya, bandari, umeme wa maji, reli, mifumo ya umwagiliaji, madini na viwanda nchini.

 


Mchengerwa amefanya kikao kazi na wawekezaji hao ili kuwa na uelewa wa pamoja juu ya shughuli wanazozifanya, ili kuona kama kuna haja ya kushirikiana nao katika ujenzi wa mji mpya wa kisasa katika jiji la Dar es Salaam kwa kuzingatia maslahi mapana ya Taifa.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv



Post a Comment

0 Comments