TANZANIA, RWANDA, UGANDA KUSAINI MoU MRADI WA KUFUA UMEME NSONGEZI

 

Tanzania imeshiriki Mkutano wa 17 wa Baraza la Mawaziri la kisekta la Nishati, Petroli na Madini la Jumuiya ya Afrika Mashariki Februari 14, 2025, Jijini Arusha. 

 

Mkutano huo unaojadili miradi inayotekelezwa ambayo ni pamoja na mradi wa kufua umeme wa Nsongezi utakaotekelezwa na Nchi za Tanzania, Rwanda na Uganda. 

 

Baraza hilo la kisekta limekutana ambapo Mawaziri husika watasaini Hati ya Makubaliano (MoU) ya utekelezaji wa Mradi huu. 

 

Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga amehudhuria mkutano huo akimwakilisha Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko.

 

Aidha, Baraza hilo linasimamia Kongamano na Maonesho ya 11 ya Petroli ya Jumuiya ya Afrika  Mashariki ambalo litafanyika tarehe 5 hadi 7 Machi 2025 Jijini, Dar es Salaam. 

 

Uenyeji wa Tanzania katika kongamano hilo unatokana na maamuzi ya mkutano wa 16 wa Baraza la Mawaziri la Kisekta lililofanyika Mwezi Februari 2024  ambalo liliamua Tanzania kuwa Mwenyeji wa Kongamano hilo.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments