Mbunge wa Nanyamba Abdallah Chikota, ameridhishwa na maendeleo ya ujenzi wa shule ya sekondari ya kata ya Hinju, inayojengwa na serikali kwa gharama ya zaidi shilingi Milioni 560.
Chikota amefika kukagua shule hiyo leo Februari 27, 2025 katika ziara yake ya ukaguzi wa miradi huku akiwataka wakazi wa kata hiyo kuwathamini walimu waliopangwa kufundisha shule hiyo mpya.
Mkuu wa shule hiyo Fidelia Kagombe, amesema ujenzi wa shule umehusisha vyumba Vinane vya madarasa, Ofisi Mbili za walimu, Maabara Tatu, Maktaba, jengo la utawala, matundu 12 ya vyoo, kisima na kichomea taka.
Amesema shule hiyo inayojengwa kupitia mradi wa SEQUIP ina jumla ya wanafunzi 156.
#KhomeinTvUpdates
✍️ Juma Mohamed-Mtwara
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments