Vongozi wa shule ya sekondari ya Kiyanga halmashauri ya mji Nanyamba mkoani Mtwara, umelazimika kuanza masomo na wanafunzi 74 wa kidato cha kwanza wasiokuwa na sare, ili kuendana na ratiba za masomo.
Mkuu wa shule hiyo Vagrey Kidava, amesema shule yao ni mpya na imefunguliwa Februari 10, 2025, hivyo wameona ni bora waanze masomo kisha sare zitafuata baadaye.
Mbunge wa Nanyamba Abdallah Chikota, amefika kukagua shule hiyo yenye vyumba Vutatu vya madarasa na matundu Sita ya vyoo, ambayo ujenzi wake umegharimu zaidi ya shilingi Milioni
80.
Amesema changamoto za uhaba wa nyumba za walimu na walimu kwa ujumla zinakwenda kutatuliwa na serikali, huku akiwataka wanafunzi kuweka jitihada kwenye masomo.
#KhomeinTvUpdates
✍️ Juma Mohamed-Mtwara
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments