MITAMBO NANE KATIKA MRADI WA JNHPP IMESHAKABIDHIWA KWA SERIKALI- DKT. BITEKO


 Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe.  Dkt. Doto Biteko amesema kuwa mitambo nane kati ya tisa ya kuzalisha umeme katika mradi wa bwawa la Mwalimu Nyerere (JNHPP) tayari imekabidhiwa kwa Serikali baada ya kuwashwa na hivyo imebakia mashine moja ambayo itakuwa tayari mwishoni mwa mwezi Februari mwaka huu.

 


Aidha, Dkt. Biteko ametaja ongezeko la wadau ambao wapo tayari kwa ajili ya kuboresha upatikanaji wa umeme Afrika na kupelekea Benki ya Dunia kutoa ahadi ya dola za kimarekani bilioni 22, Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) dola bilioni 18.2, Benki ya Maendeleo ya Kiislamu dola bilioni 2.7, Benki ya Maendeleo ya Asia dola bilioni 1.5, Benki ya Maendeleo ya Ufaransa dola bilioni 1 na wafadhili wengine lukuki. 

 

Dkt. Biteko ameyasema hayo Januari 31, 2025 Bungeni - Jijini Dodoma

 

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️ Ofisi ya N.W.M-Dodoma

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv



Post a Comment

0 Comments