EAJF, MANISPAA KINONDONI KUUNGA MKONO NISHATI SAFI KUPITIA MICHEZO NA BURUDANI

 

Jukwaa la Waandishi wa habari Afrika Mashariki kwa kushirikiana na Ofisi ya Manispaa ya Kinondoni  linatarajia kufanya tamasha la kuunga mkono ajenda ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya Nishati Safi ya Kupikia.

 

Tamasha hilo lililopewa jina la  "Bata la Nishati" litafanyika Februari 8, 2025 katika eneo la Mbweni Round about ya Ndege Beach Uwanja wa Mpira Jijini 

Dar es salaam lengo likiwa ni kuhamasisha matumizi ya Nishati safi na salama ya kupikia.

 

Hayo yamebainishwa  Februari 01, 2025 na Mratibu wa tamasha hilo Steven Nchimbi wakati akizungumza na Waandishi wa habari Jijini Dar es Salaam. 

 

Nchimbi amesema  kuwa tamasha hilo litakua la aina yake huku likitarajiwa kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali pamoja na Wananchi.

 

Aidha Nchimbi amesema kuwa tamasha hilo limeandaliwa kwa lengo la kuunga mkono ajenda ya Serikali ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya Matumizi ya Nishati safi na salama ya kupikia, na kuwataka wananchi kuachana na Matumizi ya Nishati chafu inayosababisha athari za Kiafya, Mazingira na hata kusababisha vifo.

 

Vilevile Nchimbi ameongeza kuwa ili kuendana na malengo ya Dunia ya kukabiliana na hali ya mabadiliko ya tabia nchi yatokanayo na hali ya kutohifadhi Mazingira, ni vyema kuachana na matumizi ya Nishati Chafu. Pia amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi na kununua t-shirts na kofia kwa ajili ya tamasha hilo, kwa gharama ya shilingi shilingi elfu 35,000/-

 

Nchimbi ameuhabarisha umma kuwa," Tamasha hilo litakuwa na mbio za Marathon kilometa 2.5 pamoja na kilometa 5,  zoezi la upimaji wa afya bure, burudani ya muziki mubashara kutoka bendi ya FM Academia inayoongozwa na  Patcho Mwamba, pamoja na kuchoma nyama bure kwa kutumia Nishati safi, hivyo wananchi naomba mjitokeze kwa wingi."

 

Namba ya kulipia ni 16154388 jina ni M.B.I ONLINE TV au kupitia benki ya CRDB namba 0133914590500 jina ni EAST AFRICA JOURNALIST FORUM.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️ Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments