Mteule wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, Dkt. Haji Mnasi Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Siha na Mwandishi wa kitabu cha Elimu na Malezi kwa Watoto katika Zama Za Kidijitali amezindua kitabu hicho katika kijiji cha Kitangari Sokoni kilichopo wilayani Newala mkoani Mtwara.
Uzinduzi wa kitabu hicho umefanyika hivi karibuni, katika uzinduzi huo Dkt.Mnasi amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa namna anavyotoa fedha nyingi za kutekekeza miradi nchini.
Pia amesema, kwa upande wake, licha ya kuwa na majukumu mengi ya kiserikali lakini aliwiwa kuandika kitabu hicho cha Elimu na Malezi kwa Watoto katika zama za kidigitali kutokana na kasi kubwa ya ukuaji wa utandawazi ambao kwa kiwango kikubwa unaathiri Mila na Tamaduni katika Jamii yetu, hivyo kitabu hicho kinaenda kuwa suluhisho katikati zama hizi za utandawazi na ukuwaji wa teknolojia.
Dkt. Mnasi amewataka wazazi, walezi pamoja na Jamii kupata nakala za kitabu hicho ili kuwasaidia watoto katika namna bora ya kujifunza na kupata elimu pamoja na malezi yaliyo bora ili kukuza Taifa lenye maadili mema na uchapakazi.
✍️Mwandishi wetu
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments