Wadau wa Sekta ya Utalii mkoani Arusha wamemshukuru Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa maono yake ya kuanzisha Royal Tour ambayo imekuwa na matokeo Chanya katika kukuza Utalii Mkoani Arusha, kupitia biashara ya Mahoteli.
Hayo yameelezwa Mkoani humo na Meneja Utawala wa Hoteli ya Kitalii ya PALACE, Joseph Mremi , katika hafla ya kupongezana kwa Menejimenti ya hoteli hiyo pamoja na kumuunga Mkono Rais Samia Suluhu Hassan kwa kazi kubwa ya kukuza utalii Arusha, iliyofanyika hotelini hapo na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali.
“Lengo kuu la hafla hii ni kumuunga Mkono Rais wetu Dkt. Samia kwa kazi kubwa anayoifanya ya kukuza utalii kupitia Royal Tour ambayo imekuwa na tija kubwa kwetu kama wadau wa Utalii” amesema Meneja huyo.
Amesema hafla hiyo pia imelenga kuwakutanisha na wadau wengine wa Utalii ambao wamekuwa msaada mkubwa katika ustawi wa hoteli hiyo katika kujenga mahusiano ya kibiashara tangu kuanzishwa kwake miaka kumi na tano iliyopita.
“Lengo lingine lililotukutanisha hapa ni kubadilishana uzoefu na wadau wengine wa Utalii katika kukuza biashara zetu na kuitangaza Arusha”amefafanua .
Mremi amewashukuru wadau wa utalii waliojumuika katika hafla hiyo iliyoenda sanjari la kuwashukuru wafanyakazi wa hoteli hiyo kwa ushirikiano wao na kuwapa zawadi.
Hata hivyo amewataka wadau mbalimbali wa utalii mkoani Arusha kuitumia hoteli hiyo kwa ajili ya huduma mbalimbali ili kuunga mkono sekta hiyo
✍️Mwandishi wetu
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments