Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limeuteua mkoa wa Mtwara, kuwa miongoni mwa vituo mwenyeji wa Ligi ya Mabingwa wa Mikoa (RCL) hatua ya makundi, inayotarajiwa kuanza Machi 13 hadi Machi 26, mwaka huu.
Kwa mujibu wa barua ya TFF kwenda kwa Chama cha Soka Mkoa wa Mtwara (MTWAREFA) ni kwamba Mtwarefa imethibitisha utayari na uwezeshaji wa huduma zote muhimu za mashindano hayo.
Kufuatia hatua hiyo, mwenyekiti wa Chama Cha Soka Mkoa wa Mtwara (MTWAREFA) Athumani Kambi, amesema hatua hiyo ni njema kwao kama mkoa katika harakati za kupigania kuwa na timu kwenye ligi kuu ya Tanzania Bara.
Kambi ambaye amezunhumza kwa njia ya simu na Khomein Tv, amesema mkoa wa Mtwara unawakilishwa na timu ya Bandari Sc amhayo ndio mabingwa wa mkoa huo, na wameonesha nia ya dhati ya kutaka kupanda ligi kuu, hivyo kupata fursa ya kuwa mwenyeji wa mashindano hayo ni fursa kubwa kwa Bandari katika harakati za kwenda ligi kuu.
Timu Saba zilizopangiwa kituo cha Mtwara ni mwenyeji Bandari SC (Mtwara), Mnazi Mmoja Rangers (Lindi), The Mighty Elephant (Ruvuma), Vijana SC (Njombe), Tanesco Iringa (Iringa), Nyika SC (Pwani) na Bara FC (Dar es Salaam).
Ikumbukwe kuwa, mkoa wa Mtwara uliwahi kuwa mwenyeji wa ligi ya mabingwa wa mikoa wakati huo ikiitwa ligi ya Taifa, ndipo ambapo safari ya Ndanda kupanda ligi kuu ilipoanzia.
#KhomeinTvUpdates
✍ Juma Mohamed
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments