Mbunge wa Jimbo la Mbarali Mkoa wa Mbeya, Bahati Ndingo amegawa mitungi ya nishati ya safi ya gesi kwa Mama lishe 100 kutoka maeneo mbalimbali wilayani humo.
Ndingo amekabidhi mitungi hiyo, Februari Mosi, baada ya kuwa Mgeni Rasmi katika Maadhimisho ya miaka 48 ya kuzaliwa kwa Chama cha Mapinduzi (CCM) yaliyo andaliwa na Jumuiya ya Umoja wa Wanawake (UWT) .
Ndingo amesema lengo la kutoa nishati hiyo ni kuunga mkono juhudi za Rais Samia Suluhu Hassan, katika kuhamasisha wananchi kutunza mazingira na kugeukia matumizi ya nishati safi ili kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi.
Katika hatua nyingine, Ndingo kwa kushirikiana na wajumbe wa Umoja wa wanawake UWT, wametoa misaada mbalimbali kwa wanafunzi 27 wenye mahitaji maalumu katika Shule ya Msingi Igomelo .
Pia wametoa mahitaji mengine yakiwemo mashuka, sabuni, mafuta na vifaa vya kuwasitili watoto kwenye Wodi ya Wazazi Hosptali ya Wilaya katika kuhitimisha maadhimisho ya kuzaliwa kwa CCM wilayani humo.
Ndingo amesema kampeni ya ugawaji nishati ya gesi ni endelevu lengo ni kuona jamii inaachana na matumizi ya kuni na mkaa ambayo sio salama kwa afya zao.
Baadhi ya Mama lishe wameshumshukuru Mbunge huyo kwa hatua ya kuwagusa kwani anakwenda kuokoa afya ya watu wengi ambao wamekuwa wakipata madhara kutokana na matumizi ya mkaa na kuni.
✍️ Mwandishi wetu-Mbeya
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments