RAIS SAMIA AZINDUA SERA YA ELIMU|AZITAKA WIZARA KUSIMAMIA KIKAMILIFU


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, Februari 01, 2025 amezindua Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014 Toleo la 2023, pamoja na mitaala iliyoboreshwa katika ngazi ya Elimu ya Awali, Elimu ya Msingi, Elimu ya Sekondari na Elimu ya Ualimu.

 

Uzinduzi huo umefanyika jijini Dodoma katika ukumbi wa Jakaya Kikwete Convention Center ambapo Tanzania imeandika historia.

 

katika uzinduzi huo Rais Samia amesema kuwa, uamuzi huu wa kihistoria wa kuboresha sera na muundo wa elimu ya Tanzania unakusudia kulipatia Taifa vijana wenye elimu bora zaidi, wanaojiamini zaidi, na wenye nyenzo stahiki kushindana kikanda na kimataifa. 

 

Ameongeza kuwa, Kazi ya msingi ya ujenzi wa miundombinu inayobeba utekelezaji wa sera na mabadiliko haya inaendelea, ambapo katika kipindi cha mwaka 2021 hadi 2024 zimejengwa shule mpya za msingi 1,649, shule mpya za sekondari 1,042, vyuo 64 vya ufundi stadi (VETA) katika wilaya 64 ambazo awali hazikuwepo. 

 

Hatahivyo, Rais Samia ameelekeza Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Wizara ya Fedha, Wizara ya Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) na Wizara ya Mipango na Uwekezaji kusimamia kikamilifu utekelezaji wa mabadiliko haya ili yaweze kuleta manufaa yanayokusudiwa.

 

Amesema kuwa, Utekelezaji huu uende sambamba na kupitia upya maslahi ya kada ya ualimu nchini ili kuipa hadhi inayostahili kama mama wa taaluma zote duniani.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️ Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv



Post a Comment

0 Comments