Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amefanya uhamisho wa Wakuu wa Wilaya wawili na uteuzi wa viongozi mbalimbali.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Dkt. Moses Kusiluka leo Februari 21, 2025 ni kwamba, uhamisho wa Wakuu wa wilaya umehusisha Mhe. Dkt. Vicent Nano Anney aliyehamishwa kutoka Wilaya ya Bunda kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Maswa.
Uhamisho mwingine ni wa Mhe. Aswege Enock Kaminyoge aliyehamishwa kutoka Wilaya ya Maswa kwenda kuwa Mkuu wa Wilaya ya Bunda.
Aidha, Rais Dkt. Samia amemteua CPA Juma Ajuang Kimori kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Ukaguzi na Usimamizi wa Vyama vya Ushirika (COASCO). CPA Kimori anachukua nafasi ya Bw. Yona Killagane ambaye amemaliza muda wake.
Mwingine ni Prof. Edward Gamaya Hoseah alieteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Hospitali ya Benjamin Mkapa. Prof. Hoseah anachukua nafasi ya Dkt Deo Mtasiwa ambaye amemaliza muda wake.
Uteuzi mwingine ni wa Bi Renatha Munda Rugarabamu alieteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF). Bi Rugarabamu anachukua nafasi ya Bw. Emmanuel Humba ambaye amemaliza muda wake.
Jaji Mstaafu Awadh Mohammed Bawazir ameteuliwa kuwa Mwenyekiti wa
Mamlaka ya Rufani ya Zabuni za Umma (PPAA). Jaji Mstaafu Bawazir anachukua
nafasi ya Jaji Mstaafu Sauda Mjasiri ambaye amemaliza muda wake, huku Balozi Ramadhani Muombwa Mwinyi akiteuliwa kuwa Mwenyekiti wa Baraza la
Vongozi la Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa Dkt. Salim Ahmed Salim kwa kipindi
cha pili.
#KhomeinTvUpdates
✍️Juma Mohamed
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments