SERIKALI YA AWAMU YA SITA YASHIRIKIANA NA ITALY KUVUTIA WAWEKEZAJI

 

Wawekezaji, maafisa wa serikali na wadau wa biashara zaidi ya 500, wameshiriki kongamano la Uwekezaji kati ya Tanzania na Italy lililoanza Februari 11, 2025 jijini Dar es Salaam katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC).

 

Kongamano hilo limekuwa fursa muhimu ya majadiliano na kubadilishana mawazo kuhusu mikakati ya kuvutia uwekezaji zaidi kati ya Tanzania na Italy.

 

Lengo la kongamano hilo lilikuwa kuimarisha ushirikiano wa kibiashara na uwekezaji katika sekta za afya, kilimo, na uchumi wa bluu.

 

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mahmoud Kombo, amesisitiza umuhimu wa ushirikiano wa kiuchumi kati ya Tanzania na Italy, huku akiwakaribisha wawekezaji wa Italy kuwekeza nchini.

 

Naye, Balozi wa Italy nchini Tanzania, Giuseppe Coppola, ameeleza kuwa Italia itaendelea kushirikiana na Tanzania katika sekta mbalimbali ili kuimarisha uchumi wa nchi zote mbili.

 

Hata hivyo, Kongamano hili limekuwa fursa muhimu ya majadiliano na kubadilishana mawazo kuhusu mikakati ya kuvutia uwekezaji zaidi kati ya Tanzania na Italy ambapo Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC) kimeshiriki.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments