Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema Serikali inaendelea kubuni mbinu mbalimbali za kukabiliana na wanyamapori wakali na waharibifu huku akiielekeza Wizara ya Maliasili na Utalii kuangalia namna ya kupitia upya kanuni za malipo ya kifuta jasho/machozi.
Ameyasema hayo Februari 24,2025 katika ziara alipokuwa akizungumza na wananchi kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Lushoto Mkoani Tanga.
"Tunaendelea kuongeza Askari Wanyamapori na kubuni mbinu mbalimbali za kufukuza wanyama ikiwemo kutumia ndege nyuki (drones)" Rais Samia amesisitiza.
Mkutano huo umehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Chama na Serikali wakiwemo Waziri wa Maliasili na Utalii, Balozi Dkt. Pindi Chana (Mb), Naibu Waziri, Mhe. Dunstan Kitandula (Mb), Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbas pamoja na baadhi ya Watendaji kutoka Wizara ya Maliasili na Utalii na Taasisi zake.
#KhomeinTvUpdates
✍️Mwandishi wetu
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments