Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Dkt. Doto Biteko Februari 11, 2025 amewasili nchini India kwa ajili ya kushiriki mikutano mbalimbali ya kimataifa ya nishati ambayo inakwenda sambamba na Maadhimisho ya Tatu ya Wiki ya Nishati ya India mwaka 2025 (India 3rd Annual Energy Week) inayoanzia Februari 11 hadi 14, 2025.
Katika Uwanja wa Kimataifa wa Indira Gandhi, jijini New Delhi, Dkt.Biteko amepokelewa na Balozi wa Tanzania nchini India, Balozi Anisa Mbega na Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Mafuta na Gesi India, Sandeep Jain.
Wiki ya Nishati India itakutanisha Mawaziri na Watendaji Wakuu wa Sekta ya Nishati kutoka maeneo mbalimbali duniani, watunga sera na wavumbuzi wa teknolojia mbalimbali za kisasa za nishati kwa lengo la kuja na mustakabali endelevu wa upatikanaji nishati. Aidha, Wiki hiyo itahusisha pia maonesho ya teknolojia mbalimbali za matumizi ya Nishati Safi ya Kupikia
Katika ziara hiyo, Dkt.Biteko ameambatana na baadhi ya Wajumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini pamoja na baadhi ya Watendaji wa Wizara ya Nishati na Taasisi zake wakiongozwa na Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu, Mhandisi Innocent Luoga.
✍️Mwandishi wetu
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments