TANZANIA YASHIRIKI MKUTANO WA BODI TENDAJI YA 156 WHO

 

Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, imeshiriki katika Mkutano wa Bodi Tendaji ya 156 ya Shirika la Afya Duniani - WHO, ulioanza  Februari 3 hadi 11, 2025  Geneva-Uswis.

 

Naibu Katibu Mkuu, Ismail Rumatila pamoja na Mganga Mkuu wa Serikali, Dkt.Grace Magembe wameongoza ujumbe wa Tanzania kwenye mkutano huo.

 

Mkutano huu unalenga kujadili ajenda mbalimbali zitakazowasilishwa wakati wa Mkutano wa 78 wa Shirika la Afya Duniani utakaofanyika Mei 2025.

 

Pia wameshiriki katika vikao vya awali ambapo, Naibu Katibu Mkuu ameshiriki kikao cha pembezoni cha kujadili Mikakati ya kujumuisha Afya ya mtu binafsi katika Afya kwa wote iliyoandaliwa na Global Self Care Federation na the United -Self Care Coalition. 

 

Aidha, Mganga Mkuu wa Serikali ameshiriki katika vikao vya awali vya Kikundi Kazi cha Afrika kwa ajili ya kuweka maandalizi ya uwasilishaji kabla ya kikao cha Mkutano wa Bodi Tendaji kuanza.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments