WATUMISHI MNAODAIWA MIKOPO ELIMU YA JUU LIPENI-DC MWAIPAYA

 

Mkuu wa wilaya ya Mtwara Abdallah Mwaipaya, amewataka watumishi ambao wanadaiwa mikopo ya elimu ya juu, kurejesha mikopo hiyo haraka ili kutoa fursa kwa wanavyuo waliopo vyuoni kunufaika na mikopo.

 

Akiwa katika kilele cha maadhimisho ya miaka 20 ya kuanzishwa kwa Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu, kwa kanda ya kusini yaliyofanyika viwanja vya Mashujaa Manispaa ya Mtwara-Mikindani leo Februari 11, 2025, Mwaipaya amesema viongozi wa taasisi wanatakiwa kutoa ushirikiano kwa Bodi ya Mikopo, kuhakikisha watumishi wanafanya marejesho hayo.

 


“Inawezekana na sisi leo tuna watoto tunahitaji waende vyuo vikuu, na tunataka waende vyuo vikuu na wanahitaji kupata hiyo mikopo,sasa wakati mwingine mnaizuia hiyo mikopo, na mimi niseme tu wakati mwingine muwe mnaangalia kama kuna mtu anaomba halafu baba zao hajarudisha hiyo mikopo, waambie mpaka baba zao warejeshe mikopo ndio mikopo waweze kupatiwa.” Amesema Mwaipaya.

 


Akitoa taarifa ya Bodi ya Mikopo katika maadhimisho hayo, ambayo yamehusisha wadau mbalimbali wakiwamo Benki ya NMB, Meneja wa Bodi ya Mikopo Kanda ya Kusini Rukia Semwaiko, amesema kiasi cha shilingi Trilioni 8.2 kimetolewa kuwakopesha wanavyuo wa vyuo mbalimbali wapatao 830,000 nchini Tanzania.

 

“Lakini vilevile katika Mtwara Kanda yetu ya Kusini, Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu inahudumia mikoa Mitatu, ambayo ni Mtwara, Lindi na Ruvuma.” Amesema Semwaiko.

 


Shija Renatus Zengo, ni mwanafunzi wa chuo cha kikuu kishiriki cha Stella Maries (STEMUCO) Mtwara, anaeleza faida wanazozipata kupitia mikopo hiyo kuwa ni pamoja na kupata pesa ya kujikimu.

 

Wadau wengine walioshiriki maadhimisho hayo ni Benki ya CRDB, Taasisi ya Uhasibu Tanzania (TIA) kampasi ya Mtwara, Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mkoa wa Mtwara na Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) Mtwara.

 

 

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️Juma Mohamed-Mtwara

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments