Ikiwa ni siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan kupitia mtandao wake wa kijamii, amewatakia Waislamu wote kheri ya mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, sambamba na kuwasihi waumini kuiombea amani nchi yetu.
Rais Dkt. Samia ameandika hayo Machi 1, 2025, kuwa; “Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema atuongoze na kutusimamia kwenye Ibada hii muhimu katika imani, aipe kibali cha kheri na kuipokea,
Katika Ibada hii na kama ambavyo tumeendelea kufanya wakati wote, tuendelee kuitunza na kuiombea nchi yetu amani,
Tuendelee kumuomba Mwenyezi Mungu atujaalie kila mmoja kwa nafasi yake kuendelea kutekeleza wajibu wake kwa uadilifu, kwa haki na kweli, na matokeo ya maisha na kazi zetu yawe yenye kumpendeza Yeye na yenye kulifaa Taifa letu na watu wake.
Ramadhan Mubarak.”
#KhomeinTvUpdates
✍️ Mwandishi wetu
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments