WIZARA YA KATIBA NA SHERIA YATOA ELIMU YA URAIA NA UTAWALA BORA LINDI

 

Wizara ya Katiba na Sheria kwa kushirikiana na Wataalamu kutoka Ofisi ya Rais-TAMISEMI, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora pamoja na Jeshi la Polisi, imeanza kutoa mafunzo ya Elimu ya Uraia na Utawala Bora, kwa viongozi na watalaamu mkoani Lindi.

 

Mafunzo hayo ambayo yatafanyika kwenye halmashauri zote za mkoa wa Lindi, yamefunguliwa leo Machi 3, 2025 mjini Lindi na Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Victoria Mwanziva.

 


Katika hotuba yake ya ufunguzi Mwanziva amesema “Wote hapa ni mashahidi wa vitendo vya uvunjwaji wa haki za binadamu na misingi ya utawala bora vinavyoripotiwa katika maeneo yetu kupitia vyombo vya habari na vingine inawezekana tumewahi kuvishuhudia vikilalamikiwa na wananchi kwenye maeneo yetu ya kazi.”

 


Ameongeza kuwa Wilaya ya Lindi ni mnufaika wa fedha zinazotolewa na serikali kuu kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali, hivyo mafunzo hayo yatasaidia kujenga misingi bora kwa watendaji katika usimamizi wa miradi hiyo, ili thamani ya fedha ionekane.

 


Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na Tathmini kutoka Wizara ya Katiba na Sheria Bw. Emmanuel Mayeji, amesema miongoni mwa malengo ya kutoa elimu ya Uraia na Utawala Bora kwa viongozi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa ni pamoja na kuwajengea uwezo viongozi wanaosimamia mamlaka hizo, wataalamu katika halmashauri na watendaji wa kata ili kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia katiba ya Tanzania.

 


Washiriki 51 wanapatiwa elimu hiyo kwa Manispaa ya Lindi, ambapo na wao wanatarajiwa kwenda kuishusha kwa viongozi wengine kwenye ngazi za mitaa katika maeneo yao

 

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️ Juma Mohamed-Lindi

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta @khomeintv_

 

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments