Watu Wanne waliokuwa wamepakiana kwenye Pikipiki Moja wamefariki dunia kwa ajali, baada ya dereva wa Pikipiki hiyo ambayo haina usajili aina Haojue kugonga gema kisha kuanguka kwenye safu ya Milima ya Miyuyu wakitokea Wilaya Newala mkoani Mtwara kwenda Nachingwea Lindi.
Taarifa ya Kaimu Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mtwara Kamishna Msaidizi wa Pilisi (ACP) Mtaki Kurwijila, imesema waliofariki kwenye ajali hiyo ni Hamza Mohamed Lwowa (28) Dereva mkazi wa kijiji cha Mtongwele, Haris Mohamed (28) mkazi wa Kijiji cha Mdamlole, Aziz Seleman (18) mkazi wa kijiji cha Mtongwele na Simon Madenge (30) mkazi wa kijiji cha Meta.
“Chanzo cha ajali hiyo ni uzembe wa mwendesha pikpiki kuendesha kwa mwendo kasi kulikopelekea kushindwa kuimudu pikipiki hiyo kwenye eneo la mteremko mkali na kona hatimaye kugonga gema na kusababisha vifo.” Imeeleza taarifa hiyo.
Mili ya marehemu imehifadhiwa Hospitali ya Mission Nanda -Masasi kwa uchunguzi na taratibu nyingine.
Katika hatua nyingine Jeshi la Polisi Mkoa wa Mtwara linamtafuta Ally Geukwa kwa tuhuma za mauaji ya Fatuma Chionda (47) Mkulima ,mkazi wa Kijiji cha Nangomba. Mtuhumiwa alitekeleza tukio hilo tarehe 02.03.2025 na kutoweka kusikojulikana.
Chanzo cha mauaji ni wivu wa kimapenzi wa muda mrefu.
#KhomeinTvUpdates
✍️ Juma Mohamed-Mtwara
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments