Katika kuelekea maadhimisho ya Siku ya Wanawake Duniani Machi 8, 2025, yenye kaulimbiu "Wanawake na Wasichana 2025: Tuimarishe Haki, Usawa na Uwezeshaji”, Wizara ya Nishati imempongeza Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa tuzo ya Goalkeeper ambayo imetambua mchango katika kupunguza vifo vya kina mama wakati wa kujifungua kwa asilimia 80 na Vifo vya watoto chini ya miaka 5 kwa kila vizazi 1,000.
Wizara hiyo inajivunia jitihada za Rais Samia katika kulinda haki, usawa na kuwawezesha wanawake, jitihada zinazofanyika nchini katika kulinda haki usawa na kuwawezesha wanawake kiuchumi kupitia nishati ya umeme na nishati safi ya kupikia.
Pongezi hizo zimetolewa na Naibu Waziri wa Nishati, Judith Kapinga alipokuwa akieleza ni namna gani Wizara ya Nishati inakwenda kuadhimisha Siku ya Wanawake Duniani.
"Tumepeleka umeme kwenye zaidi ya Vitongoji elfu 33, lakini kupitia nishati safi ya kupikia kupitia programu mbalimbali tumepeleka mitungi takribani Laki Nne na Ishirini majiko banifu laki 2 pamoja na majiko ya umeme." Amesema Kapinga
Ameeleza kuwa jitihada zote za Serikali katika uwekezaji sekta ya nishati hususani nishati safi ya kupikia zinalenga kuboresha ustawi wa mwanamke na kuongeza thamani yake katika kujihusisha na shughuli za maendeleo katika jamii.
Aidha, Kapinga amesema kuwa kupitia Sera ya Elimu Bure kumekuwa na ongezeko la idadi ya wanafunzi wa kike mashuleni, aidha uboreshaji katika sekta ya afya umewafanya wanawake wapate uhakika wa kuendelea na shughuli za uzalishaji kutokana na upatikanaji wa matibabu sahihi.
#KhomeinTvUpdates
✍️ Mwandishi wetu
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments