Migogoro ya ardhi inayohusisha wakulima na wafugaji, ni miongoni mwa changamoto kubwa zinazowakabili baadhi ya watendaji wa kata wa Halmashauri ya wilaya ya Kilwa mkoani Lindi.
Moja ya vikwazo vikubwa kwa watendaji hao katika kukabiliana na changamoto hizo, ni uelewa duni wa masuala ya kisheria yanayohusu utatuzi wa migogoro hiyo, na kujikuta wanatekeleza majukumu yao katika mazingira magumu.
Wizara ya katiba na Sheria wakiwa na Wataalamu kutoka ofisi ya Rais-TAMISEMI, Tume ya Haki za Binadamu na utawala Bora pamoja na Jeshi la Polisi, wametia timu wilayani Kilwa na kutoa elimu ya Uraia na Utawala bora, kwa watendaji hao na baadhi ya wakuu wa idara na Vitengo wa halmashauri pampja na Kamati ya Usalama ya wilaya.
Mafunzo hayo, yamefunguliwa na Mkuu wa Wilaya ya Kilwa Mohamed Nyundo, ambaye amekiri kuwa wilaya ya Kilwa inakabiliwa na changamoto mbalimbali zinazohitaji msaada wa kisheria katika utatuzi, hususani masuala ya migogoro ya ardhi.
Miongoni mwa watoa mada kwenye mafunzo hayo, ni pamoja na Kamishna Msaidizi wa Polisi Elisante Ulomi, kutoka jeshi la Polisi Tanzania, ambaye ametoa elimu ya Ulinzi na Usalama wa Nchi kwa washiriki wa mafunzo hayo.
Jumla wa washiriki 42 kutoka halmashauri ya wilaya ya Kilwa wakiwamo watendaji kata, baadhi ya wakuu wa idara na vitengo wa halmashauri na kamati ya ulinzi na usalama, wamepatiwa elimu ya Uraia na Utawala bora kutoka wizara ya Katiba na Sheria.
✍️ Juma Mohamed-Kilwa
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments