Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imefanikiwa kukamata Madini ya almasi yenye thamani ya zaidi ya Sh1.7 bilioni, yaliyokuwa yakitoroshwa kupitia Uwanja wa ndege wa Mwanza.
Akitoa taarifa hiyo Mei 23, 2025 Waziri wa Madini, Anthony Mavunde amesema madini hayo yalikamatwa Mei 18, 2025 kwa ushirikiano kati ya vyombo vya ulinzi na taasisi mbalimbali za Serikali na kutumia fursa hiyo kumpongeza Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Said Mtanda, Vyombo vya usalama, uongozi wa uwanja wa Ndege wa Mwanza na Kikosi Kazi cha Wizara ya Madini kwa kazi kubwa na ya kizalendo ambayo wameifanya.
“Mtu mmoja raia wa kigeni ambaye ana asili ya India , anashikiliwa kwa mahojiano kuhusiana na tukio hilo na anatarajiwa kufikishwa mahakamani uchunguzi na taratibu zitakapo kamilika.
Katika tukio hilo,almasi ghafi yenye uzito wa karati 2,729.82 na thamani ya takriban USD 635,887.66 (sawa na Shilingi za Kitanzania 1,715,434,129.67) yaligunduliwa yakiwa yamefichwa kwenye mabegi manne na raia mmoja mwenye asili ya India kwa lengo la kuyasafirisha bila vibali halali wala kufuata taratibu za kisheria.
Waziri Mavunde ametoa rai kwa wadau wote wa Sekta ya Madini nchini kuhakikisha wanafuata sheria ya biashara ya madini nchini Tanzania ili wasipate hasara kwa kupoteza madini hayo ambayo hutaifishwa na serikali.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Said Mtanda amesema Mkoa wa Mwanza unaendelea kuimarisha ulinzi na udhibiti wa biashara zote haramu ili kuhakikisha nchi yetu ya Tanzania inanufaika na rasilimali madini.
#KhomeinTvUpdates
✍️Mwandishi wetu
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments