NEEMA YA RAIS SAMIA YAWAFIKIA WANANCHI WA SAME

 

Wananchi wa Jimbo la Same Mashariki, Wilaya ya Same, mkoani Kilimanjaro, wanatarajia kunufaika na juhudi za Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kupitia mradi mkubwa wa ujenzi wa kituo cha kupokea, kupooza na kusambaza umeme katika Kata ya Maore.

 

Kwa mujibu wa Meneja wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Wilaya ya Same, Mhandisi Fabian Ruhumbika, mradi huo unatekelezwa kwa gharama ya Shilingi bilioni 3.3 na unatarajiwa kukamilika ifikapo mwezi Agosti 2025. Kukamilika kwake kutaondoa changamoto ya kukatika kwa umeme ambayo imekuwa kero kwa muda mrefu kwa wakazi wa eneo hilo.

 

Akizungumza wakati wa ziara ya Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya inayoongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Same, Mheshimiwa Kasilda Mgeni, Mhandisi Ruhumbika alieleza kuwa kituo hicho kitakuwa na uwezo wa kuongeza uzalishaji wa umeme kutoka megawati 2 hadi megawati 10. Ongezeko hilo litaongeza upatikanaji wa umeme wa uhakika, hali itakayochochea ukuaji wa uchumi, kuvutia wawekezaji, na kuanzisha viwanda pamoja na shughuli nyingine za uzalishaji.

 

Mkuu wa Wilaya, Kasilda Mgeni, alitumia fursa hiyo kumshukuru Rais Samia kwa kutoa fedha kwa ajili ya mradi huo, ambao alisema ni suluhisho la kudumu kwa changamoto ya nishati katika wilaya hiyo. Aidha, alieleza kuwa ukarabati wa kituo hicho kilichojengwa miaka ya 1980 ni sehemu ya mikakati ya Serikali ya Awamu ya Sita ya kuimarisha miundombinu ya nishati kwa maendeleo endelevu ya kijamii na kiuchumi.

 

"Mradi huu ni ushahidi tosha wa dhamira ya dhati ya Rais Samia katika kuwahudumia Watanzania wote kwa usawa. Tuna imani kuwa wananchi wa Same watanufaika na mabadiliko makubwa kiuchumi kutokana na mradi huu,” alisema Kasilda.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments