Mashindano ya "Betika Tulia Marathon 2025" msimu huu yamekuja kivingine baada ya ujio wa mbio za watoto kuanzia miaka mitano na kuendelea.
Dkt. Tulia ambaye licha ya kuwa mgeni Rasmi amekuwa kivutio kwa kushiriki mbio za mita 100, za uwanjani na kushika nafasi ya kwanza, huku mbio za watoto za mita 50 alishika nafasi ya pili dhidi ya mshindi wa kwanza Diana John (6).
Akizungumza na waandishi wa habari Dkt. Tulia amesema ushiriki wa mashindano ya msimu huu ni mkubwa na mikakati katika msimu ujao ni kutupia jicho mbio za uwanjani.
Amesema wanajivunia msimu huu mwamko ni mkubwa sana na kubainisha fedha za ushiriki zinazopatikana zinaelekezwa kwenye miradi ya sekta ya elimu na afya katika Mkoa wa Mbeya.
"Pia kupitia mashindano haya tumeweza kutoa mahitaji kwa wanafunzi wa mazingira magumu na ujenzi wa makazi ya wazee wasio jiweza ambapo tunatarajia kukabidhi nyumba tatu kesho baada ya kuhitimishwa kwa mbio za "Betika Tulia Marathon 2025,"amesema.
Mratibu wa mashindano hayo Lwiza John ameomba wadau kuunga mkono mbio za uwanjani ili kuibua vipaji hususani kwa watoto wadogo.
#KhomeinTvUpdates
✍️Mwandishi wetu-Mbeya
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments