KENYA KUENDELEA KUHESHIMU MAMLAKA YA TANZANIA

 



Mei 20, 2025, Serikali ya Kenya kupitia Msemaji wake, Isaac Mwaura, imesema kuwa Tanzania ina haki kamili, kama nchi huru na mwanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), ya kudhibiti nani anaingia ndani ya mipaka yake. Mwaura amesema kuwa hakuna taifa jingine linalopaswa kuiwekea Tanzania shinikizo kuhusu masuala ya uhamiaji.

 

Aidha, serikali hiyo imesisitiza kuwa itaendelea kuheshimu mamlaka ya mataifa jirani na kuhimiza mazungumzo ya kidiplomasia katika kutatua masuala ya aina hiyo.

 

Hayo yamejiri baada ya baadhi ya ‘wanaharakati’ kuzuiwa kuingia nchini Tanzania baada ya kutua uwanja wa ndege wa Julius Nyerere kwa ajili kusikiliza kesi ya Mwenyekiti wa Chadema, Tundu Lisu.

 

‘Wanaharakati’ hao kutoka Kenya waliozuiliwa ni mwanasiasa wa upinzani Martha Karua na aliyekuwa Jaji Mkuu wa Kenya, Willy Mutunga. Hatua iliyozua hisia tofauti ndani ya Kenya na kwingineko.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments