Rais Mstaafu wa awamu wa Nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, amesifu maono ya Taasisi ya Thabo Mbeki ya Afrika isiyokaa kando katika maendeleo ya dunia.
Dkt. Kikwete ambaye ni Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, ameyasema hayo wakati wa mjadala wa umma ulioandaliwa na taasisi ya Thabo Mbeki kwa kushirikiana na AngloGold Ashanti, uliofanyika kwenye ukumbi wa Nkrumah katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
Akisisitiza ujumbe wa siku hiyo, Dkt. Kikwete amethibitisha kuwa moto wa Uamsho wa Afrika umechochewa tena, na kutoa wito kwa viongozi na wadau kufanya mageuzi ya kweli badala ya mabadiliko ya juu juu.
Rais wa Zamani wa Afrika Kusini Thabo Mbeki aliwataka washiriki kutafakari kuhusu umuhimu na uelewa wa sera kuu za bara, hasa zile zinazohusu maendeleo ya vijana, na kuhoji ni vijana wangapi wa Kiafrika wanafahamu sera hizo.
Mjadala huo ulihusisha mchango wa Rais wa zamani wa Afrika Kusini, Mhe. Thabo Mbeki, Rais mstaafu wa awamu ya Nnne wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Dkt. Mbuyiseni Ndlozi kutoka Bunge la Afrika Kusini, pamoja na Simon Shayo, mzaliwa wa UDSM na Makamu wa Rais wa Masuala ya Uendelevu (Afrika) katika AngloGold Ashanti.
Wanafunzi wa chuo walishiriki kwa kutoa maoni kuhusu uwezeshaji wa vijana, wakisisitiza umuhimu wa mbinu jumuishi na ushirikishwaji wa jamii katika kushughulikia changamoto zao mahususi.
Mjadala huo wa UDSM ni miongoni mwa mfululizo wa matukio kuelekea Hotuba ya Siku ya Afrika, ambayo yatakamilika kwa meza ya majadiliano ya ngazi ya juu itakayoandaliwa na AngloGold Ashanti pamoja na Rais Mbeki siku ya Ijumaa tarehe 23 Mei 2025 ikifuatiwa na Hotuba rasmi siku ya Jumamosi tarehe 24 Mei katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNICC).
#KhomeinTvUpdates
✍️Mwandishi wetu
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments