Mwenyekiti wa Bodi ya Ithibati ya Waandishi wa Habari, Tido Mhando, Mei 19, 2025 ametangaza rasmi uzinduzi wa mfumo mpya wa kidijitali wa uombaji wa Ithibati ya Kitambulisho cha Uandishi wa Habari (Press Card).
Mfumo huu unapatikana kupitia tovuti rasmi ya Bodi: https://www.taihabari.jab.go.tz.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Mhando ameeleza kuwa waandishi wa habari wote wanaotaka kupata kitambulisho hicho wanapaswa kuwa na nyaraka muhimu zifuatazo:
Picha ndogo (passport size)
Vyeti vya elimu
Kitambulisho cha Taifa (NIDA)
Barua ya utambulisho kutoka kwa taasisi anayofanyia kazi au mahali anapowasilisha kazi zake endapo ni mwandishi wa kujitegemea (freelancer)
Ada ya Ithibati ya shilingi elfu hamsini (TSh 50,000)
Mhando amebainisha kuwa baada ya kuwasilisha maombi, mwombaji atapokea ujumbe wa SMS kuonyesha hatua ya maombi yake, ikiwa ni pamoja na kama yamekubaliwa, yanahitaji marekebisho, au yamekataliwa.
Aidha, Mwenyekiti wa bodi hiyo amesema haya kwa muombaji,"endapo maombi yatakubaliwa, Bodi ya Ithibati itamjulisha mwombaji kuhusu mahali na muda wa kuchukua Kitambulisho. Kitambulisho hicho kitaweza kutumika katika maeneo yote ya kihabari, ndani na nje ya taasisi."
Aidha, amesisitiza kuwa utaratibu huu umezingatia Kanuni ya 17 ya Kanuni za Sheria ya Huduma za Habari, inayowahusu:
Wahariri, Waandishi wa kujitegemea (Freelancers na Correspondents),Watangazaji, Wapiga picha, Waandaaji wa vipindi vya habari (Producers), Wanafunzi wa vyuo vya uandishi wa habari na
Waandishi wa habari wa kigeni.
Kwa mara ya kwanza, waandishi wa habari sasa wataweza kupata Ithibati kwa njia rahisi, ya haraka na ya uwazi kupitia mfumo huu wa kisasa wa kidijitali.
✍️Mwandishi wetu
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments