HATUTOI NAFASI KIUMBE YEYOTE KUJA KUTUVURUGA KWETU-RAIS SAMIA

 


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameviagiza vyombo vya ulinzi na usalama pamoja na wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, kutoruhusu Wanaharakati kutoka nchi za nje kuingia nchini kwa lengo la kuharibu amani ya nchi.

 


Rais Dkt. Samia ametoa agizo hilo leo Mei 19, 2025 jijini Dar es Salaam, wakati akitoa hotuba ya uzinduzi wa Sera ya Mambo ya Nje ya Mwaka 2001 toleo la mwaka 2024, katika ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Julius Nyerere International Conference Center (JNICC).

 


“Tumeanza kuona mtiririko au maneno ya Wanaharakati ndani ya region yetu hii kuanza kuvamia na kuingilia mambo yetu huku, sasa kama kwao wameshadhibitiwa wasije kutuharibia huku. Tusitoe nafasi walishaharibu kwao, walishavuruga kwao nchi iliyobaki haijaharibika, watu wapo na usalama na amani na utulivu ni hapa kwetu.

 

Kuna majaribio kadhaa, niwaombe sana vyombo vya ulinzi na usalama na ninyi wasimamizi wa sera zetu, kutokutoa nafasi kwa watovu wa adabu wa nchi nyingine kuja kutovuka hapa kwetu, hapana.

 


Nimeona Clip kadhaa za kunisema nipo ‘bias’ na nini ninalofanya ni kulinda nchi yangu na ndio wajibu niliyopewa, kwahiyo hatutotowa nafasi kwa kiumbe yeyote kuja kutuvurugia hapa awe yupo ndani awe anatoka nje hatutotoa nafasi.” Amesisitiza Rais Samia.

 

Awali, akizungumza kabla ya kumkaribisha Rais Samia, Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Hussein Ali Mwinyi, akapongeza sera hiyo kuzingatia diplomasia ya uchumi wa buluu.

 


“Nitoe rai kwa wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa Afrika Mashariki, na Mabalozi wanaoiwakilisha Tanzania katika nchi na mashirika ya Kimataifa kuhakikisha kwamba Zanzibar inanufaika kikamilifu na fursa za kiuchumi na kijamii zinazopatikana kupitia ushirikiano wa Uwili, Kikanda na Kimataifa.”

 

Naye Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Mahmoud Thabiti Kombo, amesema sera hiyo itasaidia wadau wa sekta binafsi na serikali kutumia ipasavyo Balozi za Tanzania katika nchi mbalimbali.

 

#KhomeinTvUpdates

 

✍️Juma Mohamed-Dar

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv


Post a Comment

0 Comments