MBUNGE AGAWA NISHATI SAFI KWA MAMA LISHE NA BABA LISHE MAGUGU

 

 

MBUNGE wa Viti Maalum Mkoa wa Manyara. Regina Ndege amegawa majiko ya gesi kwa wanawake na wanaume wauza vyakula (mama lishe na baba lishe) wa mji mdogo wa Magugu Wilayani Babati Mkoani Manyara.

 

Mbunge huyo Regina Ndege ameendelea kuunga mkono jitihada za Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kutoa nishati safi kwa mama lishe na baba lishe wa eneo hilo la Magugu.

 

Mbunge Regina Ndege akizungumza wakati wa kukabidhi majiko hayo amesema kwa muda mrefu wananchi wamekuwa wakitegemea kuni na mkaa kama nishati ya kupikia, hali ambayo imekuwa na athari nyingi kiafya na kimazingira.

 

Amesema kwamba kwa sasa dunia imehamasika kutumia nishati safi, na Rais Samia ameonesha mfano bora barani Afrika kwa kuifanya ajenda ya nishati safi kuwa kipaumbele cha taifa.

 

"Nishati chafu si tu ina haribu afya za binadamu bali pia inachangia uharibifu mkubwa wa mazingira hivyo kupitia majiko haya ya nishatii ya gesi itasaidia kutunza mazingira," amesema Regina Ndege.

 

Amesema Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ameonesha njia kwa kuhakikisha wananchi wanapata nishati salama na rafiki kwa mazingira.

 

Pia, Mbunge huyo ametumia nafasi hiyo kueleza mafanikio makubwa yaliyopatikana kwa Serikali ya awamu ya sita inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan.

 

"Mambo mengi yamefanyika ikiwemo kupungua kwa vifo vya mama na mtoto, maboresho katika sekta ya elimu na huduma za afya ambapo sasa vituo vingi vya afya vina vifaa muhimu kama X-Ray, tofauti na hapo awali ambapo wananchi walilazimika kusafiri umbali mrefu kupata huduma hizo," amesema Regina Ndege.

 

Hata hivyo, baadhi ya wanufaika waliopatiwa majiko hayo ya nishati safi ya gesi wamemshukuru Regina Ndege kwa msaada huo wa nishati safi na kueleza kuwa utawapunguzia gharama za kuni na mkaa na kuwaepusha na magonjwa yanayosababishwa na moshi.

 

Mmoja kati ya wanufaika hao Halima Seif amesema mbunge huyo Regina Ndege amekuwa mfano mkubwa katika kusaidia jamii inayozunguka eneo hilo.

 

"Mbunge huyu Regina Ndege amekuwa mfano wa kuigaa kwa viongozi kwani amekuwa msikivu na mwenye kutatua matatizo ya jamii pindi akielezwa," amesema

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️Mwandishi wetu-Babati

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments