Katika mzunguko wa historia za Mataifa, kuna wakati ambapo hatima ya Taifa haipangwi na mikakati ya kibinadamu pekee, bali inaamuliwa na nguvu ya juu ile isiyofungwa na takwimu, minong’ono, au makundi ya ushawishi.
Ndani ya muktadha huo ndipo jina la Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan linapochomoza, si kama anatazamwa kwa sura ya kisiasa pekee, bali kama alama ya kadari, mtu aliyeinuliwa si kwa ridhaa ya wengi wetu, bali kwa ruhusu ya Mungu mwenyewe.
Ishara njema katika macho ya kisiasa, Rais Samia aliibuka kutoka nafasi ya mtumishi wa kawaida, Waziri, Makamu wa Rais hadi kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, jambo ambalo kwa wengi lilionekana kama ni bahati tu ya kisiasa.
Lakini kwa walio na mtazamo mpana, walitambua kuwa huo ulikuwa mpango uliotimia wa muda mrefu wa Kiungu.
Hakuna bahati katika utawala wa Mungu, kila kitu kinawekwa sawia, na kila nafasi hutolewa kwa sababu mahsusi.
Kuinuka kwake ni fundisho kwamba mamlaka hutoka juu, na anayepinga, asipinge mtu, bali apambane na aliye juu ya wote.
Kelele za pumba; Katika kila kizazi, huwa kuna watu wanaochukizwa na mwangaza wa wale walioinuliwa.
Ni jambo la kawaida kwa kiongozi aliyeinuliwa na Mungu kuandamwa, kubezwa, kutukanwa na hata kutishiwa.
Lakini historia inaeleza wazi, hawashindwi waliobarikiwa kwa kadari, bali hushamiri zaidi.
Wanaomdharau Rais Samia hujisahaulisha kuwa mamlaka aliyo nayo si zawadi ya mtu, bali ni dhamana kutoka kwa Mungu, na hakuna anayeweza kufuta alichoandika Muweza.
Ustahimilivu na hekima licha ya kuandamwa na maneno ya kejeli na matusi yasiyo na tija, Rais Samia ameendelea kuongoza kwa busara, subira, na dira ya kitaifa.
Amekuwa kielelezo cha uongozi usioyumbishwa na jazba, bali unaoongozwa na uzalendo na maono ya mbali.
Kauli yake ya maridhiano si udhaifu, bali ni ishara ya ukomavu wa kiroho na kisiasa.
Ni wachache waliobarikiwa kipawa hicho cha kutawala kwa kutuliza na kuunganisha Taifa badala ya kuligawanya.
Maono ya kutimiza kusudi la Ki-Mungu kwa Taifa tangu kuingia madarakani, Rais Samia ameonyesha dhahiri kuwa uongozi wake umebeba sura ya mpito, kutoka katika siasa za msuguano hadi kwenye siasa za matumaini, amefungua milango ya kidiplomasia, ameruhusu uhuru wa habari, ameinua uchumi kupitia utalii, sambamba na kuimarisha heshima ya Taifa kimataifa na kuponya Taifa kisaikolojia.
Kazi yake ni zaidi ya majukumu ya ofisi, ambayo ni kutimiza kile ambacho pengine hakikufanikiwa kabla yake, hususani katika njia ya kuimarisha Taifa moja lenye sauti ya pamoja.
Nahitimisha kwa kusema kuwa, Rais Samia si tu kiongozi wa kisiasa, bali ni sauti ya wakati, ishara ya mabadiliko ya kihistoria, na chombo cha mpito wa Taifa.
Anayejiinua kupinga nafasi hiyo ya Rais Samia kwa hila, njama, utovu wa nidhamu, upotoshaji, ajue kuwa anajipambanua dhidi ya mpango wa Mungu.
Wakati mwingine, ukimya wa Mteule ni ushindi mkubwa kuliko makelele ya wapinzani wake.
Hivyo, wale wenye masikio ya hekima wasikie, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni chaguo la Mungu. Kadari ndio imemfikisha hapo na hakuna mwanadamu mwenye uwezo wa kupambana na muumba wake, la kama yupo basi twamkaribisha jamvini.
#KhomeinTvUpdates
✍️Mwandishi wetu
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments