Taasisi ya Vyombo vya Habari Kusini mwa Afrika, Tawi la Tanzania (MISA-TAN) kwa kushirikiana na Umoja wa Wachapishaji wa Magazeti Ulimwenguni (WAN-IFRA) na Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu Tanzania (THRDC) umeendesha mjadala kuhusu uendelevu wa vyombo vya Habari katika mawanda ya uchumi unaobadilika uliowashirikisha wadau mbalimbali wa Habari nchini.
Baadhi ya wadau hao ni wamiliki wa vyombo vya Habari, Wahariri wa Vyombo vya Habari, Wahadhiri wa Vyuo vya Uandishi wa Habari na Viongozi wa Taasisi za Habari.
Katika mjadala huo, wadau hao wa sekta ya habari walijadili mambo mbalimbali ikiwemo sheria na kanuni za uchaguzi.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa MISA Tan Edwin Soko amechangia mjadala huo na kusema, kunahitajika jitihada za pamoja kati ya Taasisi za usimamizi wa Vyombo vya habari nchini, Wamiliki wa Vyombo vya habari na waandishi wa habari kukaa pamoja kwenye kujadili uendelevu na uhimilivu wa Vyombo vya habari kwani kufanya hivyo kutasaidia kuwa na mikakati ya pamoja ya namna ya kuongeza ustahimivu wa Vyombo vya habari.
Amesisitiza pia, Jambo hilo ni muhimu sana kuliko kila upande kukaa peke yake na kubainisha changamoto wakati changamoto zinaathiri pande zote
Ameongeza Soko, MISA Tan wameanza mazungumzo na Tume Huru ya Uchaguzi kuangalia namna gani taasisi hizo zitaweza kushirikiana kuwajengea uwezo waandishi wa Habari kuhusu kanuni mpya za uchaguzi ili waweze kuzifahamu.
#KhomeinTvUpdates
✍️Mwandishi wetu
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments