WATANZANIA WANAHITAJI UMEME WA JOTOARDHI - MD TANESCO

 



Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Lazaro Twange amesema anafurahishwa na wale walioanzisha wazo hadi uwepo wa taasisi hii iliyoanzishwa mwaka 2013 kwa lengo la kuendeleza rasilimali ya jotoardhi nchini ili kuzalisha umeme. 

 

Twange ameipongeza TGDC kwa ujumla kwa utendaji kazi mzuri akitambua kuwa uanzishwaji wa jambo mpaka kuleta matokeo huchukua muda mrefu lakini hatua ni nzuri na kusisitiza kuwa Watanzania wanahitaji umeme.

 

Hayo yamejiri katika ziara ya kikazi aliyofanya Mkurugenzi huyo kuitembelea Kampuni ya Uendelezaji Jotoardhi Tanzania (TGDC) ambayo ni Kampuni Tanzu ya Shirika hilo Mei 15, 2025 kwa lengo la kuzifahamu taasisi zilizo chini ya Shirika analolisimamia.

 

Akiongea na Bodi ya Wakurugenzi, Menejimenti pamoja na watumishi akiwa katika ofisi za TGDC makao makuu, Twange. 

 


“Ninamshuruku Mheshimiwa Rais kwa kuniamini na kunipa nafasi ya kuwa mtumishi wa TANESCO na niwapongeze sana walioanzisha wazo mpaka leo tunayo TGDC. Pia niwapongeze wote kuanzia Bodi ya Wakurugenzi mpaka wafanyakazi kwa utekelezaji mzuri wa kazi.

 

Vilevile niwaambie kuwa, Watanzania wanahitaji kuuona umeme wa jotoardhi; hivyo, ninaomba sana tujitahidi, wananchi wauone umeme huu ”, amesema Twange.

 

Aidha, amemaliza kwa kusema, “nitafurahi kuwa sehemu ya shuhuda wakati wa upatikanaji wa umeme huu na niko tayari kufanya kazi na kila mmoja wenu, nitawapa ushirikiano na ninafurahi kwamba, kazi nyingi zimefanywa na wazawa. Ninatamani mjue ya kwamba, watu wanataka kuridhika na kuridhika kwao ni kuupata umeme wa jotoardhi”

 

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi TGDC Prof. Shubi Kaijage amemkaribisha na kumpongeza kwa kuteuliwa, lakini pia kwa kufika na kuwasalimu wafanyakazi na kisha kumhakikishia kuwa, maelekezo yaliyotolewa yatafanyiwa kazi na menejimenti inaendelea kutekeleza majukumu yake ipasavyo ili kuleta matokeo.

 

Awali akitoa maelezo utekelezaji wa shughuli mbalimbali ndani ya taasisi, Meneja Mkuu wa Kampuni ya TGDC Mhandisi Mathew Mwangomba alieleza kuwa, TGDC inaamini kuwa, umeme wa jotoardhi utakapozalishwa, Tanzania itakuwa imeondokana na changamoto ya upatikanaji wa umeme kwa kiasi kikubwa kupitia vyanzo mseto.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments