Mshauri wa Masuala ya Afya na Tiba wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya Taifa ya Muhimbili Profesa Mohamed Janabi, amechaguliwa kuwa Mkurugenzi wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Kada ya Afrika.
Profesa Janabi, ameshinda kinyang’anyiro hicho katika uchaguzi uliofanyika leo Mei 18, 2025 jijini Geneva nchini Uswis, kuziba nafasi ilioachwa na aliyekuwa mkurugenzi mteule wa shirika hilo Dkt. Faustine Ndungulile, ambaye alifariki duniani siku chache baada ya kutangazwa mmshindi wa nafasi hiyo.
Prof. Janabi amewashinda Dk. N’da Konan Michel Yao wa Ivory Coast, Dk. Boureima Hama Sambo wa Niger, Dk. Drame Mohammed Lamine wa Guinea na Prof. Mijiyawa Moustafa wa Togo.
#KhomeinTvUpdates
✍️Juma Mohamed
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments