USHINDI WA PROF. JANABI UNAVYOINUFAISHA TANZANIA

 

Tanzania imepata heshima kubwa ya kimataifa kufuatia uteuzi wa Profesa Mohamed Yakub Janabi, kuwa Mkurugenzi wa Kanda ya Afrika wa Shirika la Afya Duniani – WHO, kwa kipindi cha mwaka 2025 hadi 2030. 

 

Ushindi huu umetajwa kuwa sio tu ushindi wa kitaifa, bali ni fursa ya kipekee kwa taifa kunufaika kwa njia mbalimbali katika sekta ya afya na diplomasia ya kimataifa.

 

Ushindi wa Profesa Janabi unaongeza hadhi ya Tanzania katika jumuiya ya kimataifa, hasa ndani ya mashirika ya Umoja wa Mataifa. 

 

Kwa mara nyingine, Tanzania inaonekana kama nchi yenye wataalamu wenye uwezo wa kuongoza taasisi kubwa za dunia, jambo linaloweka nchi katika nafasi ya kuaminika na kuheshimiwa kimataifa.

 

Kwa upande wa maendeleo ya afya, Tanzania inaweza kunufaika kwa karibu zaidi na miradi ya WHO, ikiwa ni pamoja na mipango ya kupambana na magonjwa ya milipuko, kuboresha huduma za afya ya msingi, pamoja na kuongeza usaidizi wa kitaalamu na kifedha katika sekta ya afya. 

 

Kufuatia ushindi huo, Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, amempongeza Profesa Janabi, huku akieleza kuwa uzoefu wake katika sekta ya afya, anastahili kuliongoza bara la Afrika na kuelekea mafanikio kwenye sekta hiyo.

 

Rais Samia amewashukuru wanachama wote wa nchi wanachama waliotambua uwezo, uzoefu na maono ya Profesa Janabi kwa ajili ya bara la Afrika.

 

#KhomeinTvUpdates

 

✍️Juma Mohamed

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments