TANESCO YAMPA HEKO RAIS SAMIA KUTOA DOLA MIL. 6.4 MRADI WA MBAGALA

 

Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) limeendelea kuchanja mbuga katika utekelezaji wake ili kuhakikisha wananchi wanapata umeme wa uhakika maeneo yote nchini.

 

Mkurugenzi Mtendaji Lazaro Twange amesema wananchi wa maeneo ya Mbagala na viunga vyake sasa wanatarajia kupata umeme wa uhakika baada ya Kituo cha kupokea na kupoza umeme cha Mbagala kuongezewa uwezo kutoka Megawati 45 za awali na kufikia Megawati 165.

 

Aidha, Mkurugenzi huyo amemshukuru Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kutoa kiasi cha fedha Dola za Kimarekani milioni 6.4 ili kufanikisha Mradi huu wenye tija na manufaa kwa wananchi wa maeneo hayo na nchi kwa ujumla.

 

Twange amezungumza hayo baada ya kutembelea Kituo na kusema kuwa, Kituo hicho kimeongezewa uwezo mara mbili ya awali hivyo kitakuwa na uwezo mkubwa wa kusambaza umeme na kuondoa kabisa changamoto ya kukatika kwa umeme katika maeneo hayo.

 

“Kituo hiki kimeongezewa uwezo mara mbili ya awali na mpaka sasa utekelezaji wa Mradi huu umefikia asilimia 70. Wananchi wa Mbagala na viunga vyake sasa wategemee umeme wa uhakika’’ amesisitiza Twange.

 

Naye, Mkuu wa Wilaya ya Temeke Sixtus  Mapunda, akizungumza wakati wa ziara hiyo amepongeza jitihada zinazofanywa na TANESCO ambapo amefafanua kuwa kukamilika kwa Mradi huo kutasaidia kumaliza kero ya umeme katika maeneo mengi ya Mbagala, Temeke na Mkuranga.

 

“Kwa namna ya pekee tunaishukuru sana TANESCO kwa mradi huu, kwa awamu ya kwanza Mradi huu ulipaswa kujaribiwa mwezi Juni mwaka huu lakini Mradi umeweza kuonesha mafanikio kabla ya wakati kutokana na jitihada kubwa zinazofanywa’’ amefafanua Mapunda

 

Uboreshaji wa Mradi huu wa Kituo cha Kupokea na Kupoza na Kusambaza umeme cha Mbagala umegharimu Dola za Kimarekani milioni 6.4 ambapo sasa umefikia asilimia 70 ya utekelezaji wake na kukamilika kwake kunatarajia kusambaza umeme wa Megawati 165.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments