WAWEKEZAJI SEKTA YA MADINI WAKARIBISHWA MTWARA

 

Wawekezaji katika Sekta ya Madini wamekaribishwa kuwekezwa katika mkoa wa Mtwara kutokana na uwepo wa madini ya aina mbalimbali yakiwemo madini mkakati yanayotumika kwenye shughuli za viwanda.

 

Hayo yameelezwa na Mhandisi wa Migodi Mwandamizi, Michael Mtatiro kwa niaba ya Afisa Madini Mkazi wa Mkoa huo, Winnifrida Mrema kupitia mahojiano maalum na wanahabari wanaoandaa kipindi maalum cha kuangazia mafanikio katika Sekta ya Madini.

 

“Yapo madini mbalimbali yakiwemo yanayotokana na mchanga wa bahari (Heavy mineral sands) yanayohusisha madini ya Rutile, Titanium, Ilminite na Zircon” amesema Mtatiro.

 

Akielezea hali ya makusanyo katika mkoa huo, Mhandisi Mtatiro amesema kuwa, Mkoa wa Mtwara ulipangiwa kukusanya Shilingi Bilioni 9.18 kwa mwaka wa fedha 2024/2025, na kuongeza kuwa hadi sasa wamefanikiwa kukusanya Shilingi Bilioni 7.14 sawa na asilimia 75 ya lengo lililopangwa.

 

“Tuna imani mpaka mwisho wa mwezi wa sita tutakuwa tumefikia lengo la asilimia 100 la makusanyo,” amesema.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments