Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameanza rasmi safari kuelekea Jijini Dodoma, Makao Makuu ya Serikali, akitokea Jiji la Dar es Salaam. Safari hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yake ya Kitaifa, ambapo anatarajiwa kuhudhuria na kuhitimisha shughuli muhimu za Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Katika safari hiyo, Rais Samia ametumia usafiri wa treni ya kisasa ya mwendo kasi (SGR), akielekea Dodoma kwa ajili ya kuhutubia na kufunga rasmi Bunge la 12 , Juni 27, 2025.
Kupitia ujumbe aliouandika katika mtandao wake wa kijamii, Rais Samia amesema:
“Hotuba hiyo ni ya kihistoria na ya kipekee, kwani inahitimisha muhula wa Bunge hili ambalo limekuwa na mchango mkubwa katika kuendeleza ajenda ya maendeleo ya Taifa letu. Ni fursa ya kutathmini tulikotoka, mafanikio yaliyopatikana, changamoto tulizokutana nazo, na mwelekeo wa Taifa letu katika miaka ijayo.”
Aidha, Rais Samia ameeleza kuwa anajivunia kushiriki katika hatua hiyo muhimu ya mchakato wa kidemokrasia na uimarishaji wa utawala bora nchini, akishirikiana na viongozi wenzake, wabunge, na wananchi kwa ujumla katika kuijenga Tanzania iliyo na mshikamano, haki na ustawi kwa wote.
Rais pia ametoa shukrani kwa wananchi kwa kuendelea kuiunga mkono serikali na juhudi zake mbalimbali, akisema:
“Nawashukuru Watanzania wote kwa kuendelea kuunga mkono jitihada za serikali na taasisi zake katika kuimarisha misingi ya utawala bora na maendeleo jumuishi.”
Ziara hii ya Rais Samia inajenga taswira endelevu ya uongozi makini unaojikita katika misingi ya uwazi, uwajibikaji, na maendeleo kwa manufaa ya Watanzania wote.
#KhomeinTvUpdates
✍️Mwandishi wetu
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments