TANZANIA KUTOATHIRIKA MOJA KWA MOJA NA UMOJA WA BRICS

 

Serikali imesema kuwa Tanzania haitapata athari za moja kwa moja kutokana na mafanikio au changamoto zozote katika Umoja wa BRICS (Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini), zinazoweza kutokea katika sekta ya kiuchumi na fedha hususani ya kujiondoa kwenye Dolarisation kwa kuwa sio nchi mwanachama wa BRICS.

 

Hayo yamesemwa bungeni jijini Dodoma na Naibu Waziri wa Fedha, Hamad Hassan Chande (Mb), alipokuwa akijibu swali la Mbunge Zahor Mohammed Haji (Mwera), aliyeuliza faida na hasara ya Tanzania kutokana na msimamo wa nchi za BRICS ambazo zimejipanga kujiondoa kwenye mfumo wa Dolarisation.

 

Amesema Serikali ya Tanzania imekuwa na ushirikiano wa muda mrefu na nchi za BRICS (Brazil, Russia, India, China na Afrika Kusini) katika nyanja mbalimbali ikijumuisha masuala ya kiuchumi, biashara na diplomasia kwa kuendelea kuwepo kwa balozi za nchi hizo hapa nchini na Tanzania kuwa na balozi katika nchi hizo.

 

’’Kwa sasa Tanzania sio mwanachama wa BRICS ila inashiriki katika mikutano ya BRICS kama observer, hivyo mafanikio au changamoto zozote katika umoja huo zinazoweza kutokea katika sekta ya kiuchumi na fedha hususani ya kujiondoa kwenye Dolarisation, hatutakuwa na athari za moja kwa moja kwa kuwa sio wanachama wa BRICS,’’ almefafanua Chande.

 

Amesema mahusiano ya Tanzania na nchi hizo yanadumishwa kwa kuendelea kuwepo kwa balozi za nchi hizo hapa nchini na Tanzania kuwa na balozi katika nchi hizo.

 

Ameongeza kuwa mahusiano hayo yanaendelea kuleta mafanikio chanya kwa Serikali ya Tanzania kwa kutumia fursa za kiuchumi zinazopatikana katika nchi hizo ambazo pia zinaimarisha mahusiano ya uwili baina yake (bilateral engagement).

 

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️Mwandishi wetu

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments