Kijana Nature Willson (18) Mkazi wa Mtaa wa Mwasote Kata ya Itezi Jiji la Mbeya aliyekwama kujiunga kidato cha tano kutokana na ukata wa fedha amefutwa machozi na Spika wa Bunge, Dk Tulia Ackson baada ya kubeba jukumu la kuwatunza na kuwasomesha yeye na mdogo wake Patrick Willson (8).
Nature amehitimu kidato cha nne Sekondari Itezi jijini hapa na kuchaguliwa kujiunga kidato cha tano katika Shule ya Sekondari ya Wavulana ya Rungwe baada ya kupata ufauru wa daraja la kwanza na pointi 13 , huku wakiishi mazingira magumu na kulelewa na bibi yao Lucia Kapangali (65) ambaye ajiwezi kiuchumi.
Uamuzi wa Dkt. Tulia ambaye pia ni Rais wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), kuchukua jukumu la kuitunza na kuisomesha familia hiyo
ni baada ya kuibuliwa na mbio za bendera ya upendo iliyokimbizwa hivi karibuni kupitia Taasisi yake ya Tulia Trust.
Bendera hiyo ililenga kuzifikia kaya zenye mazingira magumu na kutoa mahitaji mbalimbali ikiwepo chakula ,mavazi na ujenzi wa makazi.
Dkt. Tulia amesema hayo jana Julai 12 , mwaka huu na kwamba pamoja na kuihudumia mahitaji muhimu, pia amechukua jukumu la kuwasomesha watoto wote wa familia hiyo, akiwemo kijana Nature aliyehitimu kidato cha nne na kupata ufaulu wa daraja la kwanza la alama 13 na kushindwa kuanza masomo ya kidato cha tano kutokana na ukata wa fedha.
Kwa upande wake, kijana Nature Wilson, ameeleza namna alivyopitia ugumu katika safari yake ya masomo ikiwa ni pamoja na kukata tamaa ya kuendea kidato cha tano baada ya familia kukosa fedha.
"Tunaishi maisha magumu kuna wakati tunalala bila kupata chakula,lakini tulikuwa tunamuomba Mungu ambaye amemleta Spika wa Bunge Dkt Tulia kutufuta machozi na magumu tunayopitia," amesema
Naye Bibi familia hiyo, Lusia Kapangala(65) amemshukuru Dkt. Tulia pamoja na wananchi kwa kuwa msaada kwao katika kipindi chote.
#KhomeinTvUpdates
✍️Mwandishi wetu-Mbeya
PIA USIACHE KU SUBSCRIBE
CHANEL YETU Khomein TV
YOUTUBE UWE WA KWANZA
KUFIKIWA NA HABARI ZETU
Follow Insta & Threads @khomeintv_
Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok
@khomeintv na Facebook Khomein Tv
0 Comments