SERIKALI KUHAKIKISHA KILA MTANZANIA ANAPATA HUDUMA BORA ZA AFYA

 

Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan imedhamiria kuhakikisha kuwa kila Mtanzania anapata huduma bora za afya katika utekelezaji wa dhana ya Afya moja.

 

Hayo yamebainishwa Julai 11, 2025 Jijini Dodoma na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia Afya Prof. Tumaini Nagu wakati akitoa uelekeo juu ya Mkutano Mkuu wa Mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri unaotarajiwa kufunguliwa rasmi Julai 12, 2025.

 

Prof. Nagu amesema mkutano huo muhimu utatoa wigo wa kuweka mikakati ya pamoja ili kuendelea kuboresha huduma za afya kutokana na uwekezaji mkubwa wa miundombinu uliofanywa na Rais wa Jamhuri  ya Muungano wa Tanzanaia Dkt.Samia Suluhu Hassan.

 

“Mipango ya Serikali kwenye msingi wa Afya  kwa wote ni kuhakikisha kila Mtanzania anapata huduma bora za afya kwani Rais amefanya uwekezaji mkubwa katika sekta ya afya,”amesema Prof. Nagu.

 

Aidha, Prof.Nagu amesema watatumia kikao hicho kutafakari nini kimefanywa hivyo ni sehemu ya kusherehekea mafanikio ya Serikali ya awamu ya sita ndani ya sekta ya afya ambapo zaidi ya Shilingi Trilioni 1.3 ziliwekezwa kwa njia mbalimbali kwenye afya ya msingi ikiwemo miundombinu na vifaa tiba.

 

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Serikali Dkt. Grace Magembe ametoa wito kwa Wakuu wa Taasisi za Sekta ya Afya kuhakikisha wanaandaa miongozo ya kugundua magonjwa mapema na kuzuia .

 

“Sisi wote ni sekta moja, wakuu wa taasisi miongoni mwa majukumu yenu ni eneo la utafiti na kuandaa miongozo ya kugundua magonjwa mapema na kuzuia, “amesema Prof. Nagu.

 

Mkutano wa Mwaka wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri mwaka 2025 umeanza Julai 11 hadi 13, 2025 na unatarajiwa kufunguliwa rasmi Julai 12, 2025 na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan huku ukienda sambamba na kaulimbiu isemayo ”Wajibu wa Waganga Wakuu wa Mikoa na Halmashauri katika Kuimarisha Ubora wa Huduma za Afya kuelekea Bima ya Afya kwa Wote.

 

#KhomeinTvUpdates 

 

✍️Juma Mohamed-Dar

 

PIA USIACHE KU SUBSCRIBE

CHANEL YETU Khomein TV

YOUTUBE UWE WA KWANZA 

KUFIKIWA NA HABARI ZETU

 

Follow Insta & Threads @khomeintv_

Tufollow pia kwenye X (Twitter), TikTok

@khomeintv na Facebook Khomein Tv

Post a Comment

0 Comments